Kila asubuhi nilipokuwa naamka nilihisi kizunguzungu cha ghafla na wakati mwingine vidole vya mikono na miguu vilikuwa vinakufa ganzi. Mara nyingi nilibaki kitandani nikiogopa kusimama ghafla kwa sababu nilihisi dunia ikizunguka na mapigo ya moyo kwenda kasi isiyo ya kawaida.
Watu wa familia yangu walidhani labda ni uchovu wa kawaida lakini ndani yangu nilijua kitu hakiko sawa. Niliishi na hofu ya kufa ghafla kila siku kwa sababu nilishaanza kusikia visa vya watu kuanguka na kupoteza maisha kwa shinikizo la damu.